Msaada: Kuanzisha ukurasa mpya

From mediawiki.org
This page is a translated version of the page Help:Starting a new page and the translation is 100% complete.
PD Kumbuka: ukifanya mabadiliko kwenye ukurasa huu, umekubali kutoa mchango wako chini ya kifungu CC0. Tazama Kurasa za Msaada wa Kikoa cha Umma kwa habari zaidi. PD

Kuna njia kadhaa za kuanza ukurasa mpya.

Hizi zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya ukurasa ulioanza, pamoja na wiki na umaarufu wa manenoakiba(en, reserved words).

Kutumia viungo vya ndani

MediaWiki inafanya iwe rahisi sana kuunganisha kurasa za wiki kwa kutumia mifumo ya kawaida (angalia Help:Links ).

Kama wewe (au mtu mwingine yeyote) umeunda kiungo cha makala ambayo haipo bado, kiungo kitakuwa na rangi nyekundu, kama hii.

Maelezo::
  • sampuli hii inaonyesha kuimarisha mtindo bila masharti. kupigiwa mstari kumeonyeshwa hapo chini ya maandishi ya viungo halisi kimsingi itafichwa kama chaguo msingi na kuonekana tu wakati kiunga kimeguswa au kuchaguliwa na urambazaji wa kibodi, ikiwa wiki (au upendeleo wa mtumiaji) imetumia chaguo msingi la Wiki. :* Rangi halisi ya viungo pia inategemea mitindo msingi ya wiki (default), na muundo wa kurasa za Wiki bado unaweza kuondoa rangi msingihizi(default).

Unapobofya kiungo chenye rangi nyekundu, kitakuchukua mpaka kwenye ukurasa wa kuhariri makala mpya.

Kwaurahisi tu andika maandhishi yako, bonyeza Hifadhi na ukurasa mpya utaundwa.

Mara baada ya ukurasa kuundwa, kiungo kitabadilika kutoka nyekundu hadi bluu (kijani cha zambarau kwa kurasa ambazo umezuru) kuonyesha kwamba makala sasa ipo.

Kwa kawaida hii ni njia bora ya kuunda ukurasa mpya, kwa sababu inamaanisha kwamba tangu mwanzo, ukurasa utaunganishwa kutoka angalau mahali pengine kwenye wiki (na kawaida unataka kuunganisha kwenye kurasa zingine zinazohusiana baadaye).

Ikiwa unaanzisha ukurasa mpya bila kuunganisha na sehemu yeyote, unapaswa kujiuliza: Je, ukurasa huu unalingana na mada ambazo tayari zimezungumziwa kwenye wiki?

Vile vile, ni kwanamna gani wageni na watu wengine wataupateje ukurasa huu?

Kwa kawaida nivigumu kuunda ukurasa bila kwanza kuunda kiungo chekundu kwa maada husika.

Kutoka kwenye sanduku la Utafutaji

Kama utafuta ukurasa ambao haupo, basi utapewa kiungo cha kuunda ukurasa mpya.

Kwakutumia URL

Unaweza kutumia URL ya wiki kwa kuunda ukurasa mpya.

URL ya makala katika wiki inafanana na kitu kama hiki:

  • http://www.example.net/index.php/ARTICLE    or
  • http://www.example.net/wiki/ARTICLE

Kama utabadirisha MAKALA kwa jina la makala unayo taka kuunda, utapelekwa kwenye ukurasa mtupu ikiashiria kwamba hakuna makala yenye jina kama hilo ambayo iko tayari.

Ukibofya "Hariri" page tab juu ya ukurasa wako itakuppeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa kuhariri, ambapo utaandika maandishi yako ya ukurasa mpya kisha utaboya kusanya(submit)

Kwakutumia Kigezo cha kuunda Makala

Njia hii inahitaji Extension:InputBox kusakinishwa.

Nakili maandishi yafuatayo kwenye ukurasa katika wiki wiki:

<inputbox>
type=create
width=100
break=no
buttonlabel=Create new article
default=(Article title)
</inputbox>

Hii hutoa sanduku ambapo watumiaji wanaweza kuandika tu kichwa cha makala na kuunda ukurasa wenye jina hilo.

Hii huwawezesha wahariri wasio na uzoefu kuunda kurasa kwa urahisi.

Kuunda mwelekezo kwenye Ukurasa Mpya

Usisahau kuweka mwelekezo ukiunda Ukurasa mpya.

Ikiwa unafikiri mtu mwingine anaweza kutafuta ukurasa ulio uanzisha kwa kutumia jina au maneno tofauti, tafadhali weka mwelekezo sahihi.

Angalia Help:Redirects .

Kulinda ukurasa wako Mpya

Kwa kawaida ukurasa mpya wa wiki unaweza kuhaririwa na watu wengine (hiyo ni moja ya wazo kuu ya wiki!).

Hata hivo watu maalumu protect wanaweza kulinda kurasa ili watu wakawaida wasiweze kufanyia marekebisho kwenye ukurasa huyo.