Ukuaji/Majarida/29
Jarida la timu ya ukuaji #29
Karibu kwenye jarida la ishirini na tisa kutoka kwa Timu ya Ukuaji! Msaada wa tafsiri
Mazungumzo ya Jumuiya
Timu ya Ukuzaji itaandaa mazungumzo yake ya kwanza ya jumuiya Jumatatu, 4 Desemba (19:00 - 20:30 UTC). Mada ya mkutano huu itakuwa Unasihi.
Mkutano wa kwanza wa Lugha utakuwa kwa Lugha ya Kiingereza, lakini tunapanga kuandaa mazungumzo katika lugha zingine, na kuhusu mada zingine. Tafadhali tembelea ukurasa wa mazungumzo kwenye-wiki kwa maelezo kuhusu jinsi ya kujiunga. Unaweza pia kutazama ukurasa, au kupendekeza mawazo kwa mazungumzo yajayo hapo.
Moduli ya Athari
Mwanzoni mwa Novemba 2023, timu ya Ukuaji ilituma Moduli Mpya ya Athari kwenye Wikipedia zote. Hivi majuzi tulitoa uboreshaji wa ufuatiliaji wa jinsi data ya kuhariri ilivyoonyeshwa kulingana na maoni ya wahariri. [1]
Ongeza Kiungo
Tulitoa “ongeza kiungo” kwa Wikipedia 35 zaidi. [2] [3]
Tuna Wikipedia chache zilizosalia:
- Wikipedia ya Kijerumani na Kiingereza tutawasiliana nazo mwanzoni mwa Januari 2024.
- Kuna miradi michache ya wiki ambayo haitapokea jukumu hilo hadi iwe na makala za kutosha ili algorithm ifanye kazi vizuri.
Usanidi wa Jumuiya
- Tulishirikisha mipango ya Usanidi wa Jumuiya 2.0 na wadau wa mambo ya kiufundi. [4] 🖂
- Mawazo ya muundo wa Usanidi wa Jumuiya ya awali yamekwisha shirikishwa na kujadiliwa na wanajumuiya.
- Onesho la msingi la la Usanidi wa Jumuiya 2.0 linatolewa kwenye ToolForge.
- Wasanidi programu wanaweza kupata uthibitisho wa awali wa msimbo wa dhana iliyoshirikishwa kwenye gitlab.
Unasihi
Wakati mnasihi atakapoweka alama kuwa "Hayupo", majina yao yalikuwa hayapangiwi akaunti mpya waliporudi. Hili limerekebishwa. [5]
Tuliboresha ujumbe uliokuwa ukipokelewa na wageni wakati mnasihi wao anaacha kazi, ili kupunguza mkanganyiko. [6]
Tulilifanyia kazi jambo la kuhakikisha kwamba washauriwa wote wamepewa mshauri hai. Hii ilihitaji kugawa upya washauriwa waliokuwa hawana washauri kwa mshauri mpya. Tulisitisha hili kwani hati ya kusafisha iliwachanganya baadhi ya wahariri. Tutaianzisha tena wakati vizuizi vilivyotambuliwa vitakapotatuliwa. [7]
Sasa inawezekana kuunda Kichujio cha Matumizi Mabaya ili kuzuia mtumiaji mmoja kujisajili kama mshauri. [8]
Jarida la timu ya ukuaji lililotayarishwa na timu ya Ukuaji na kuchapishwa na bot • Toa maoni • Jisajili au ujiondoe.